Our use of cookies

We use cookies to give you the best possible experience on our site. By continuing to use the site you agree to our use of cookies.


Analytics cookies

We’d like to set Google Analytics cookies to help us to improve our website by collecting and reporting information on how you use it. The cookies collect information in a way that does not directly identify anyone.

:


Kabanga Nickel Yapata Leseni Maalumu ya Uchimbaji Madini

Kabanga Nickel Yapata Leseni Maalumu ya Uchimbaji Madini

Mambo Muhimu

  • Leseni maalum ya uchimbaji madini imetolewa kwa ajili ya Mradi kabanga Nickel na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Ni Leseni Maalumu ya uchimbaji Madini ya kwanza kutolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha miaka kumi.
  • Pamoja na makubaliano ya mfumo wa uendeshaji wa kampuni na kuhamisha Idhini ya Mazingira, Mradi uko katika nafasi ya kipekee ya kuendelezwa.
  • uidhiniswa/ Kutolewa kwa Leseni hii ni uthibitisho na Imani kwa Mradi na watendaji wake
  • Watendaji wa makao makuu pamoja na wale wa kambini wako tayari kwa shughuli za awali za mradi.

Dodoma, London, 27 Oktoba, 2021, Kabanga Nickel Limited (“Kabanga Nickel”) inayo furaha kutangaza kuwa Tembo Nickel Corporation Limited, mbia wetu na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, imepatiwa Leseni Maalumu ya Uchimbaji wa Madini (“SML”) kwa mradi wa Kabanga Nickel (“Mradi”). Leseni Maalumu ya Uchimbaji madini imetolewa kufuatia utiliaji Saini Makubaliano ya mfumo wa uendeshaji wa kampuni yaliyofanyika mwezi wa Januari 2021 na utakuwa hai kwa kipindi chote cha maisha ya mradi huu (kwa sasa ni zaidi ya miaka 33).

Kwa sasa Kabanga itaharakisha uendelezaji wa Mradi ambao ni moja kati ya hifadhi kubwa duniani ya madini ya Nikeli Salfaidi ambayo haijachimbwa, na ni madini muhimu sana katika undelezaji na utengenezaji wa betri zinazotumika kwenye magari yanayotumia mfumo wa umeme. Mahitahi ya betri za magari ya umeme yataongeza uhitaji mkubwa wa madini ya nikeli kwa kipindi kifupi kijacho.

Mheshimiwa Dotto Biteko, Waziri wa Madini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema:

“Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ninayo furaha kutangaza kuidhinishwa kwa Leseni Maalumu ya Uchimbaji Madini kwa Tembo Nickel, Mradi wa Kabanga Nickel. Kwa makubaliano ya mfumo wa uendeshaji wa kampuni na Kibali cha Mazingira kilichohamishwa, Kabanga Nickel sasa amekamilisha taratibu za udhibiti kuanza kuendeleza mradi huo. Katika uzalishaji, Kabanga atakuwa mzalishaji muhimu wa madini ya nickel, na mipango ya madini nchini Tanzania, Tanzania itakuwa mshirika muhimu katika soko la kimataifa la nickel. Ikiwa na makisio ya miaka 30 ya uhai wa mgodi, Kabanga ina nafasi ya kuleta faida za kijamii na kiuchumi kwa kizazi kipya cha watanzania”.

Chris Showalter, Afisa mtendaji mkuu wa Kabanga Nikeli alisema:

“Kutolewa kwa Leseni Maalumu ya Uchimbaji Madini kwa Kabanga ni ishara ya wazi na Imani kwa Mradi na watendaji wake toka kwa washirika wetu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunatambua mchango wao na mchango wa washirika wengine wote katika kuendeleza mradi huu. Kwakuwa sasa tunayo Leseni, shughuli za uendelezaji mradi ambazo tayari zinafanyika katika mradi wa Kabanga sasa zitaongezeka kwa kasi kubwa. Kabanga itakuwa muhimu katika uendelezaji na usambazaji wa mahitaji makubwa ya madini ya kutengenezea betri, ambayo ni muhimu kwa mabadiliko ya tabia nchi kuelekea uchumi usio hatarishi kwa dunia. Matumizi ya www.kabanganickel.com 2 teknolojia ya uchenjuaji “hydrometallurgy” kuzalisha bidhaa bora iliyokamilika hapa nchini, itahakikisha kwa kiasi kikubwa uzalishaji salama na endelevu, na wakati huo huo ikiongeza thamani nchini Tanzania.

Leseni Maalumu ya Uchimbaji Madini imeidhinishwa na Baraza la Mawaziri na kutiwa sahihi na Tume ya Madini ikiwa na baraka zote za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Leseni hii inaiwezesha kampuni mwenza, Tembo Nickel kuwa na haki za madini ambazo zitafungua fursa kubwa za kiuchumi za mradi wa Kabanga Nickel.

Kwa kutolewa kwa Leseni Maalum ya Uchimbaji Madini na Makubaliano ya Mfumo wa Kampuni kuidhinishwa na Serikali ya Tanzania, watendaji wa kambini pamoja na wahusika wa mahusiano ya kijamii wamekwisha tayarishwa na wataelekeza juhudi zao katika ukarabati wa kambi, kuwezesha shughuli kamili za uendelezwaji wa Mradi.