Our use of cookies

We use cookies to give you the best possible experience on our site. By continuing to use the site you agree to our use of cookies.


Analytics cookies

We’d like to set Google Analytics cookies to help us to improve our website by collecting and reporting information on how you use it. The cookies collect information in a way that does not directly identify anyone.

:


Kampuni ya Kabanga Nickel yapokea fedha za uwekezaji wa dola za Kimarekani milioni 50 kutoka kwa Kampuni ya BHP

Mambo Muhimu

  • Kabanga ni eneo lenye hazina kubwa zaidi ya Nikeli Salfaidi kote duniani. Ikiwa magharibi mwa Tanzania, Kabanga ina madini ya nikeli ambayo haijachimbwa yanayokadiriwa kufikia takribani tani milioni 1.86 na nikeli daraja la kwanza kwa kiwango cha 3.44%1,2.
  • Ratiba ya mradi inakadiria uzalishaji kuanza mnamo mwaka 2025, kiwango cha chini cha uzalishaji wa nikeli kikikadiriwa kuwa tani 65,0002 kwa mwaka, huku mradi ukikadiriwa kuwa na uhai wa takribani miaka zaidi ya 30 ya utafiti na uchimbaji.
  • Uwekezaji wa dola za Kimarekani milioni 40 kutoka BHP, kampuni inayoongoza duniani katika uchimbaji wa madini, utaharakisha ujenzi wa Mradi wa Kabanga Nickel wa kuzalisha nikeli ya Daraja la Kwanza ya kiwango cha kutengenezea betri, madini ya kobalti na shaba.
  • Uwekezaji zaidi wa Dola za Kimarekani milioni 10 kutoka BHP utaendeleza teknolojia kutoka Lifezone inayotumia kiwango kidogo cha hewa ya ukaa kupitia teknolojia ya uchenjuaji ijulikanayo kama hydrometallurgy ambayo ni ya gharama nafuu zaidi kuliko teknolojia ya kuyeyusha (smelting) na ina athari ndogo katika mazingira.
  • Makubaliano yamefanyika ambapo yatategemea vigezo kadhaa kuhusu sehemu nyingine za uwekezaji ndani ya Kabanga Nickel, ikiwa ni pamoja na awamu ya pili ya Dola za Kimarekani milioni 50 na haki ya BHP ya kufanya uwekezaji zaidi baada ya kufikia hatua zilizokubaliwa.
  • Uwekezaji huu hautahamisha haki za uendeshaji na usimamizi wa mradi kutoka kwa Kabanga Nickel Corporation kupitia kampuni ya ubia hapa nchini ya Tembo Nickel Corporation.
  • Tanzania itanufaika kikamilifu kwa uzalishaji wa madini yenye ya kiwango cha kutengenezea betri bila kutumia teknolojia ya kuyeyusha. Serikali ya Tanzania ina asilimia 16 ya hisa kupitia kampuni ya ubia hapa nchini, Tembo Nickel Corporation, na Kabanga Nickel Ltd ya Uingereza inamiliki hisa zilizobaki.

Dodoma, London, 10 Januari 2022 Kabanga Nickel Limited (“Kabanga Nickel”), kampuni Binafsi iliyosajiliwa Uingereza, inayo furaha kutangaza kwamba BHP, kampuni inayoongoza duniani katika uchimbaji wa madini, imewekeza dola za Kimarekani milioni 40 katika kampuni ya Kabanga Nickel. Fedha hizo zitatumika kuharakisha ujenzi wa Mradi wa Kabanga Nickel (“Mradi”) nchini Tanzania, eneo lenye hazina kubwa zaidi ya Nikeli Salfaidi ambayo haijachimbwa. Sambamba na hilo, BHP imewekeza dola milioni 10 za Kimarekani katika kampuni ya Lifezone Limited (“Lifezone”) ili kukuza usambazaji wa teknolojia yake yenye hatimiliki katika uchenjuaji wa madini iitwayo “hydrometallurgy” (“hydromet”). Teknolojia ya hydromet kutoka Lifezone ni ya gharama nafuu zaidi kuliko uchenjuaji kwa kuyeyusha, ina athari ndogo zaidi katika mazingira, na itahakikisha kuwa madini ya nickel yanayotumika kutengeneza betri, madini ya shaba na kobalti yanazalishwa nchini Tanzania.

Chris Showalter, Mkurugenzi Mtendaji wa Kabanga Nickel, alisema: "Tuna furaha kutangaza ushirikiano huu na BHP. Ushirikiano huu unaonyesha jinsi madini yaliyopo Kabanga yalivyo na hadhi kimataifa na umuhimu wake katika kusaidia kukabiliana na changamoto ya hewa ya ukaa inayokabili dunia hivi sasa. BHP ni mshirika sahihi kwa Kabanga Nickel, kwa kuwa ina mbinu na utaalamu mkubwa utakaowezesha mradi kusonga mbele. Uwekezaji wa BHP unadhihirisha sifa za www.kabanganickel.com | www.lifezone.tech 2 mipango na sera za Mazingira, Jamii na Utawala (Environmental, Social and Governance - ESG) za mradi na umuhimu wake katika kulinda mazingira katika mnyororo wa thamani wa nikeli. Kwa kuongezea, ufadhili wa BHP katika teknolojia ya uchenjuaji ya hydromet kutoka Lifezone, ambayo ni suluhisho la uchenjuaji endelevu wa madini, utasukuma harakati za uhifadhi wa mazingira. Kupitia ujenzi wa Kabanga na teknolojia ya hydromet kutoka Lifezone, Tanzania itakuza nafasi yake katika uzalishaji wa madini yanayotumika kutengeneza betri ambayo ni muhimu katika kufikia uchumi wa dunia wenye kiwango cha chini cha hewa ya ukaa.”

Muamala

Muamala huo ni wa jumla ya dola za Kimarekani milioni 50, ikiwemo uwekezaji katika Kabanga Nickel (Dola za Kimarekani milioni 40) na Lifezone (Dola za Kimarekani milioni 10).

Makubaliano yamefanyika ambapo yatategemea vigezo kadhaa kuhusu sehemu nyingine za uwekezaji ndani ya Kabanga Nickel, ikiwa ni pamoja na awamu ya pili ya Dola za Kimarekani milioni 50 na haki ya BHP kufanya uwekezaji zaidi baada ya kufikia hatua zilizokubaliwa.

Uwekezaji katika kampuni ya Kabanga Nickel

BHP itawekeza dola za Kimarekani milioni 90 katika hati fungani zinazoweza kubadilishwa (unsecured convertible securities) ndani ya Kabanga Nickel katika awamu mbili:

Uwekezaji wa awali wa Dola za Kimarekani milioni 40, ukifuatiwa na uwekezaji mwingine wa dola milioni 50 baada ya makubaliano kufanyika na kutimizwa kwa masharti mengine. Baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria hapa Tanzania, Awamu ya kwanza ya Dola za Marekani milioni 40 itabadilishwa na kuwa asilimia 8.9 ya hisa za Kabanga Nickel (Asilimia 7.5 ya faida za Tembo Nickel Corporation (“Tembo”).

Baada ya kuwekezwa na kubadilishwa kuwa hisa, fedha za awamu ya pili Dola za Kimarekani milioni 50 zitaongeza hisa za BHP katika KNL kufikia asilimia 17.8 (Asilimia 15.0 ya faida za Tembo), na hivyo kufanya thamani ya mradi huo kufikia dola za Kimarekani milioni 658.

Baada ya kukamilika kwa masharti mengine, BHP itapata haki ya kufanya uwekezaji zaidi katika Kabanga Nickel baada ya kufikia hatua zilizokubaliwa.

Uwekezaji huu hautahamisha haki za uendeshaji na usimamizi wa mradi kutoka kwa Kabanga Nickel Corporation kupitia kampuni ya ubia hapa nchini ya Tembo Nickel Corporation.

Uwekezaji katika kampuni ya Lifezone

Sambamba na uwekezaji ndani ya Kabanga Nickel kwa kiasi cha Dola za Kimarekani 40, BHP itawekeza dola milioni 10 katika kampuni ya Lifezone Limited. Lifezone ndiye mmiliki wa teknolojia ya uchenjuaji ya hydromet na hakimiliki husika ambazo zitatumika kujenga na kuendesha mradi wa uchenjuaji nchini Tanzania. Teknolojia ya Lifezone ya hydromet husaidia katika utunzaji wa mazingira, kupunguza kiwango kinachozalishwa cha hewa ya ukaa, na bidhaa zenye kiwango kikubwa cha faida na kuwezesha Tanzania kunufaika kikamilifu na madini nchini.

Matumizi ya mapato

Uwekezaji kutoka BHP katika kampuni ya Kabanga Nickel utasaidia kuharakisha ujenzi wa mgodi, ikiwemo kuimarisha kwa mpango wa uchimbaji madini ili kuwezesha maboresho ya Utafiti Thabiti wa Upembuzi Yakinifu na kusaidia mipango ya ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji kwa teknolojia ya hydromet unaotegemewa kukamilika. Shughuli zingine zitakazopewa kipaumbele ni www.kabanganickel.com | www.lifezone.tech 3 uhamishaji wa wananchi kutoka katika eneo la mgodi, maandalizi ya awali ya ujenzi wa mgodi ikiwemo utengenezaji wa barabara za mgodi, eneo la makazi ya wafanyakazi, ujenzi wa visima vya maji na miundombinu ya umeme. Uwekezaji huo pia utasaidia kuajiri na kutoa mafunzo kwa Watanzania.

Uwekezaji katika kampuni ya Lifezone unaruhusu kufanyika kwa maombi mapya ya hakimiliki, mbali na hakimiliki za kimataita zaidi ya 100 zilizopo, pamoja na kazi ya Utafiti na Maendeleo ambayo itasaidia zaidi katika kukuza soko la teknolojia ya hydromet kutoka Lifezone. Uzalishaji wa madini ya metali (base and precious metals) unazidi kupendelea matumizi ya teknolojia ya hydromet katika uchenjuaji, ambayo tayari inatumika katika shughuli mbalimbali duniani. Muhimu zaidi, teknolojia hii inatumia kiwango kidogo cha nishati na kupunguza kiwango cha athari kwenye mazingira.

Ratiba ya sasa ya ujenzi wa mradi inatarajia kuwa uzalishaji utaanza kufanyika mwaka 2025. Uzalishaji utaongezeka kufikia lengo la uzalishaji wa tani 40,000 za nikeli, tani 6,000 za shaba na tani 3,000 za kobalti kwa mwaka.

Kwa ushirikiano na Tanzania

Tanzania imedhamiria kuwa mzalishaji mkubwa wa madini endelevu ili kukidhi ongezeko la mahitaji duniani na kuwezesha harakati za kueleka kwenye uchumi wenye kiwango kidogo cha hewa ya ukaa. Serikali ya Tanzania ni mshirika muhimu katika ujenzi wa mradi jumuishi wa Kabanga kwa manufaa ya pande zote. Katika hotuba yake kwenye Mkutano wa COP26 mjini Glasgow Novemba mwaka jana, Rais Samia Suluhu Hassan alisisitiza haja ya nchi zilizoendelea kulisaidia bara la Afrika katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Ubia kati ya Kabanga na serikali, na ushirikiano kutoka BHP ni mfano wa namna ambayo azma hii inaweza kufikiwa.

Mheshimiwa Dr. Doto Biteko, Waziri wa Madini, alisema: “Tanzania ina ndoto ya kuwa kitovu cha madini yanayowezesha kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa. Ninafurahi kwamba Kabanga Nickel inatambua fursa hii na inawekeza katika mustakabali wetu. Kupitia kazi ya Kabanga Nickel, na rasilimali zetu wenyewe, sasa tuko tayari kuweka mchango wetu duniani katika uzalishaji na usafishaji wa metali muhimu zinazohitajika katika jamii, huku tukizalisha ajira na kukuza uchumi wa nchi yetu”

Taarifa za Ziada